Zifahamua Sifa na Bei ya Moto Z4
Simu hii mpya ya motorola inakuja na kamera ya nyuma ya Megapixel 48
Ukiangalia simu hii kwa mbele inakuja na kioo cha inch 6.4 kilicho tengenezwa kwa teknolojia ya FHD+ OLED, kioo ambacho pia kinakuja na uwezo wa resolution wa hadi pixel 1080 x 2340.
Kwa nyuma simu hii inakuja na kamera moja yenye uwezo wa Megapixel 48, kamera hiyo inauwezo wa kuchukua video za kawaida za 1080p pamoja na video za 4K.
Kwa mujibu wa motorola, Moto Z4 inategemea kupatikana kuanzia tarehe 6 mwezi ujao na inategemewa kuja ikiwa na vifaa mbalimbali ambavyo vinaitwa moto mods huku bei ya simu hiyo ikiwa ni dollar za marekani $499, sawa na takribani shilingi za kitanzania Tsh 1,148,000 bila kodi.