Zifahamu Sifa na Bei ya Simu Mpya ya TECNO Pouvoir 3
Simu hii imezinduliwa hivi karibuni huko nchini Nigeri
Kama unavyojua simu za Tecno Pouvoir zime tengenezwa maalum kwa ajili ya wale wanaopenda simu zenye uwezo wa kudumu na chaji hivyo Pouvoir 3 inakuja na battery kubwa ya 5000 mAh yenye uwezo wa kudumu na chaji kwa zaidi ya siku moja kulingana na matumizi yako.
Kwa mbele Pouvoir 3 inakuja na kamera ya Megapixel 13 ambayo inasaidiwa na Flash ya LED kuweza kupiga picha za selfie vizuri hasa wakati wa usiku.
Kwa nyuma simu hii pia inakuja na kamera ya Megapixel 13 ambayo nayo inasaidiwa na Flash mbili za LED, Vile vile Pouvoir 3 inaendeshwa na processor ya Mediatek MT6739 ambayo inasaidiwa na RAM ya GB 2 pamoja na ukubwa wa ndani au ROM ya GB 16 au GB 32.
TECNO Pouvoir 3 inakuja na ukubwa wa Kioo Inch 6.2 chenye teknolojia ya IPS LCD capacitive touchscreen display, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 720 x 1500 pixels.
TECNO Pouvoir 3 inakuja ikiwa inauzwa kwa takribani shilingi za kitanzania Tsh 350,000.