Njia Mpya ya Kutengeneza Kipato Kupitia WhatsApp
Feature hii mpya inampa uwezo mmiliki wa channel kujiingizia kipato kutokana na channel aliyofungua
Whatsapp wametangaza Mabadiliko mapya kwenye upande wa channel ambayo inaitwa Channel Subscription, hii ni feature mpya ambayo inampa uwezo mmiliki wa channel kujiingizia kipato kutokana na channel aliyofungua.
Kupitia kutengeneza maudhui ambayo ni Exclusive Content ambayo mtu ili aweze kusoma inampasa alipie ndo aweze kupata hiyo huduma. Mtu akilipia ataweza kukaa siku 30 bila kulipia tena kwa kuweza kupata makala mbalimbali baada ya kulipia.
Utaweza kuona alama ya diamond ya blue juu kabisa kwenye hiyo channel ambayo itakua unaweza kuifungua na kusoma exclusive content baada ya kulipia huduma hiyo. Huu ni mkakati wa Whatsapp kuhakikisha watengeneza maudhui wanajiingizia kipato kutokana na kazi zao.