Mtandao wa Instagram Kuja na Njia ya Kurudisha Akaunti Iliyo Dukuliwa
Ni muhimu kuwa na barua pepe au namba ya simu ili kutumia sehemu hiyo
Kwa mujibu wa tovuti ya Vice, Instagram imeanza kufanya majaribio ya sehemu hiyo ambayo itakuwa inatumia barua pepe na namba ya simu kuweza kurudisha akaunti ya instagram iliyodukuliwa.
Kwa mujibu wa tovuti VICE, watu wengi hudukuliwa akaunti zao za instagram kwa kubofya kwenye barua pepe inayotumwa na mdukuaji inayo fanana na barua pepe kutoka Instagram, barua pepe hiyo inakutaka kubadilisha password huku ikidai kuwa kuna mtu alikuwa akitaka kudukua akaunti yako.
Hata hivyo pale unapo bofya kwenye barua pepe hiyo na kuweka password zako ndio hapo mdukuaji huweza kupata password zako na kudukua akaunti yako. Sasa kupitia sehemu hiyo mpya, Instagram itakuwa inatuma barua pepe au meseji yenye tarakimu sita ambazo zitasaidia kurudisha akaunti yako, hata hivyo kama mdukuaji amedukua barua pepe yako basi instagram itahakikisha mtu atoweza kutumia tarakimu hizo kama hatumii kifaa ambacho kilitumika kutengeneza akaunti usika.