Jinsi ya Kutumia Android Kwenye Kompyuta Bila Ku-install
Tumia android kwenye kompyuta kwa urahisi (Njia ya Haraka)
MAHITAJI
Unahitaji kuwa na USB Flash yenye angalau GB 2, Unahitaji kuwa na Internet (Bando) angalau GB 1.5 au zaidi, Unahitaji kuwa na kompyuta inayotumia mfumo wa Windows, kuanzia Windows 7, 8 na 10.
HATUA
1. Kitu cha kwanza unacho takiwa kufanya ni kutembelea tovuti hii hapa ( https://url.tanzaniatech.one/BIv ), kisha download mfumo wa Android Live moja kwa moja kwenye kompyuta yako.
2. Baada ya hapo tembelea tovuti ya Rufus ( https://url.tanzaniatech.one/OGv ) kisha pakua mfumo wa rufus, mfumo huu unakusaidia kuweza kutengeneza File za mfumo ambazo zipo booted.
3. Chomeka USB Flash kisha baada ya hapo washa programu ya Rufus kama Administrator, kisha chagua USB flash uliyo chomeka kutoka kwenye kompyuta yako kwa kuchagua kwenye list ya (Device) inayo onekana juu upande wa kushoto.
4. Baada ya hapo chini kwenye (Boot selection) bofya kitufe cha Select kilichopo upande wa kulia kisha chagua mahali ulipo hifadhi file la Android ulilo pakua kwenye hatua ya kwanza. Bofya open kuweka file hilo kwenye programu ya Rufus.
5. Baada ya kuhakiki hatua zote zime enda sawa, sasa moja kwa moja bofya Start na subiri baada ya muda mfupi programu ya Rufus itakuwa imemaliza.
6. Baada ya hapo funga programu ya Rufus pia hakikisha una restart kompyuta yako na chagua boot kwa kubofya F12 au ESC kwenye kompyuta yako kisha chagua jina la Flash yako.
7. Subiria utaona mfumo wa Android utaweza kuwaka moja kwa moja kupitia kwenye Flash yako. Hongera sasa utaweza kutumia Android kwenye kompyuta yako bila kuintsall mfumo huop kwenye kompyuta yako.
