Jinsi ya kufuta kwa Haraka Picha na Mafaili Yaliyojirudia
Kama umepiga picha mbili zinzofanana na utaka kufuta moja, au kama una mafaili mengi ambayo hayana kazi basi njia hii ni bora
Ni kweli kwamba kila mtu amewahi kupiga picha na kujikuta kuna picha nyingine zinazofanana, hii inatokea mara nyingi kama umeona picha ya kwanza haijatokea vizuri na hivyo ukalazimika kupiga picha nyingine mbili ama nne zinazofanana ili kuweza kupata picha moja unayo iyopenda zaidi.
Lakini kutoka na kufanya hivi mara nyingi simu inaweza kujaa haraka sana tena hasa kama wewe ni mpenzi wa kupiga picha kwenye simu yako, kuliona hili ndio maana leo nimekuletea njia rahisi na za haraka za kuweza kupata na kufuta picha zilizo jirudia kupitia simu yako ya Android kupitia HAPA.
Njia hizi ni rahisi sana na huna haja ya kupoteza muda mwingi bali unacho hitaji ni kufuata hatua hizi chache na moja kwa moja utaweza kuzipata picha zinazojirudia ikiwa pamoja na njia rahisi ya kuweza kufuta picha hizo kama unahitaji.